Wasira amchana Zitto Kabwe sakata la Chadema kugomea uchaguzi

Wasira ametumia jukwaa hilo kuwaambia Chadema wajitokeze hadharani wawaambie wanataka nini na kama wanashindwa kuiambia CCM basi waiambie Tume.

Mar 31, 2025 - 14:55
 1  8

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amemjibu kiongozi mstaafu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa CCM haibishani na Chadema kwa kuwa iliwaambia wazungumze wakajibu hawako tayari kupotezewa muda.

Wasira ametumia jukwaa hilo kuwaambia Chadema wajitokeze hadharani wawaambie wanataka nini na kama wanashindwa kuiambia CCM basi waiambie Tume.

Wasira amesema hayo Jumapili, Machi 30, 2025 katika mkutano wa hadhara Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu huku amemjibu Zitto ambaye akiwa Lindi alisema Wasira anajua historia, hivyo kwa nini anabishana na Chadema badala ya kuzungumza.

Amesema sio kweli kwa kuwa chama ni mwanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambacho mwenyekiti wake ni Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.

What's Your Reaction?

Like Like 1
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Angry Angry 0
Sad Sad 0
Wow Wow 1