Urusi yaionya Marekani ikiishambulia Iran, ‘moto utawaka’

Rais wa Marekani, Donald Trump alitishia Jumapili kuwa atashambulia Iran, kwa mabomu na kuiwekea vikwazo iwapo haitafikia makubaliano na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia, huku Marekani ikiongeza ndege za kivita katika eneo hilo.

Apr 5, 2025 - 13:45
Apr 5, 2025 - 13:47
 0  4
Urusi yaionya Marekani ikiishambulia Iran, ‘moto utawaka’
Rais wa Urusi akizungumza katika moja ya vikao vya ndani
Urusi yaionya Marekani ikiishambulia Iran, ‘moto utawaka’
Urusi yaionya Marekani ikiishambulia Iran, ‘moto utawaka’

Moscow. Urusi imesema kuwa vitisho vya mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya mshirika wake Iran havikubaliki huku ikaonya kuwa uamuzi wa kulishambulia Dola la Kiislamu la Iran utasababisha matokeo mabaya sana ikiwa vituo vya nyuklia vitashambuliwa.

 Rais wa Marekani, Donald Trump alitishia Jumapili kuwa atashambulia Iran, kwa mabomu na kuiwekea vikwazo iwapo haitafikia makubaliano na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia, huku Marekani ikiongeza ndege za kivita katika eneo hilo.

 Ilipoulizwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na hatari zilizopo katika hali ya sasa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema kuwa Moscow imejitolea kutafuta suluhisho la mpango wa nyuklia wa Iran kwa njia inayoheshimu haki za Tehran za kuwa na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.

 “Matumizi ya nguvu za kijeshi na wapinzani wa Iran katika muktadha wa suluhisho hili ni kinyume cha sheria na hayakubaliki,” amesema Msemaji wa Wizara hiyo, Maria Zakharova.

 “Vitisho kutoka nje vya kushambulia miundombinu ya nyuklia ya Iran vitasababisha janga lisiloweza kurekebishwa duniani. Vitisho hivi havikubaliki kabisa,” ameongeza.

 Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Iran kwa kuwa na ajenda ya siri ya kutengeneza silaha za nyuklia kwa kuongeza kiwango cha usafishaji wa Uranium kwa kiwango cha juu cha uchakataji, zaidi ya kile wanachodai kuwa kinahitajika kwa programu ya kiraia ya nishati ya atomiki.

 Tehran inasema mradi huo wa urutubishaji wa nyuklia ni kwa matumizi ya nishati ya kiraia pekee.

 Russia na Iran zilitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati wa kina Januari, ingawa hakuna kifungu cha ulinzi wa pamoja.

 Chini ya makubaliano hayo, endapo chama kimoja kitashambuliwa, kingine hakitamsaidia mshambuliaji.

 “Urusi imelaani vitisho hivyo vya Marekani dhidi ya Iran,” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Ryabkov aliambia jarida la Life. Ryabkov alisema shambulizi dhidi ya Iran linaweza kusababisha mzozo mpana zaidi wa wazi katika Mashariki ya Kati.

 “Madhara ya hili, hasa ikiwa kutakuwa na mashambulizi kwenye miundombinu ya nyuklia, yanaweza kuwa mabaya sana kwa eneo zima,” alisema Ryabkov.

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Angry Angry 0
Sad Sad 0
Wow Wow 0