Magnus auawa kisa deni la Sh1,000, Polisi yamnasa mtuhumiwa
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Alex Mkama, akizungumza leo Aprili 2, 2025, amesema tukio hilo limetokea usiku wa Machi 28, 2025.
Morogoro. Mkazi wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Jackson Katabi (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua George Magnus kisa deni la Shilingi 1,000.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Alex Mkama, akizungumza leo Aprili 2, 2025, amesema tukio hilo limetokea usiku wa Machi 28, 2025.
SACP Mkama ametaja chanzo cha ugomvi huo kuwa ni marehemu kukaidi kulipa deni alilokuwa anadaiwa na mtuhumiwa la Shilingi 1,000.
“Katika ugomvi huo marehemu alipata jeraha dogo kichwani na kupatiwa huduma ya kwanza kwenye Zahanati iitwayo Kaporo Health Service na kuruhusiwa kurudi nyumbani akiwa njiani alianguka na kupoteza maisha”, amesema SACP Mkama.
Kamanda Mkama, amesema uchunguzi wakina wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
What's Your Reaction?